Mbunge wa Nzega,
Hussein Bashe amesema anaamini Edward Lowassa hakuenguliwa kwa haki na
CCM katika mchakato wa kumpata mgombea urais wa chama hicho, na kwamba
waziri mkuu huyo wa zamani si pekee ambaye amekumbana na uonevu kama
huo.
Bashe,
ambaye ameingia bungeni kwa mara ya kwanza katika Uchaguzi Mkuu wa
mwaka jana akipeperusha bendera ya CCM, pia amesema kashfa zote
zinazoikumba Serikali hutengenezewa suluhisho kwa malengo fulani na si
kutafuta muafaka wa haki.
Kiongozi
huyo wa zamani wa Umoja wa Vijana wa CCM alisema hayo katika mahojiano
maalumu na Mwananchi yaliyofanyika jijini Dar es Salaam juzi.
Bashe,
ambaye alikuwa kambi ya Lowassa wakati wa mchakato wa kumpata mgombea
urais wa CCM, alisema ingawa hana uhusiano tena wa kisiasa na kada huyo,
anaona tukio lake kuwa ni historia ya kutotendea haki wanachama wengi
wa CCM. “Si Lowassa pekee, wako wengi,” alisema Bashe katika mahojiano
hayo.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI



Post A Comment: