Umoja wa Ulaya(EU) umeishauri Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania kupendekeza kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuunda
Serikali ya Umoja wa Kitaifa.
Balozi wa Umoja wa Ulaya hapa nchini, Van de Geer amesema kuwa anategemea mkwamo wa kisiasa kati Serikali ya Zanzibar na Chama Kikuu cha Upinzani Visiwani humo CUF kutatuliwa siku za karibuni.
Balozi de Geer amesema kuwa Umoja wa Ulaya uko kwenye mazungumzo na Serikali ya Rais John Magufuli na Umoja huo unategemea Rais Magufuli ataanzisha majadiliano kutatua mgogoro uliopo na hatimaye CUF kuingizwa kwenye Serikali ya Umoja wa Kitaifa.
Serikali ya Umoja wa Kitaifa ilifikia tamati baada ya Uchaguzi wa Marudio, tarehe 20, Machi 2016 baada ya CUF kususia uchaguzi huo kwa madai kuwa wa Oktoba 25, 2015 uliofutwa walishinda na wa marudio ulikuwa hauko kisheria na usingekuwa huru na haki.
Umoja wa Ulaya umepunguza mahusiano yake na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inayoongozwa na Dkt. Ali Mohamed Shein tangu Ujumbe wa waangalizi wa Uchaguzi kutoka Umoja wa Ulaya uliokuwa ukiongozwa na Bi. Judith Sargentini kupinga Uchaguzi wa Marudio wa Machi 20, 2016.
Chama cha CUF ambacho kinaonekana kiko tayari kwa ajili ya mazungumzo, Serikali ya Zanzibar imewahi kukaririwa ikisema kuwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa(SUK) ilishazikwa, japokuwa inatambuliwa na Katiba ya Zanzibar.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI
Post A Comment: