MTUHUMIWA wa unyang'anyi wa kutumia silaha, Salum Njwete(34), maarufu kwa jina la ‘Scorpion’, jana aliishangaza Mahakama ya Wilaya ya Ilala, baada ya kutaka iendeshe kesi yake kwa kasi anayotaka yeye.
Akiwa kizimbani kama mtuhumiwa pekee, ‘Scorpion’ alitaka asomewe
maelezo ya awali ya kesi yake japokuwa hakupewa nafasi ya kujieleza kwa
lolote.
'Scorpion' aliomba asomewe maelezo ya awali sekunde chache baada ya
Wakili wa Serikali, Chesensi Gavyole kuiambia mahakama kwamba upelelezi
wa kesi hiyo umekamilika.
Baada ya Gavyole kumaliza maelezo hayo, Hakimu Frola Haule
anayesikiliza kesi hiyo alimwambia mtuhumiwa huyo kuwa ataanza kusomewa
maelezo ya awali Novemba 30.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI



Post A Comment: