KLABU ya Simba imekubali kulipa dola za Marekani 120,000 (mabazo ni zaidi ya Sh milioni 240 kwa klabu ya Sonderjiske ya Denmark ili kumrejesha mshambuliaji wake wa zamani, Mganda Emmanuel Okwi.


Baada ya klabu hiyo kukamilisha kulipa kiasi hicho cha fedha, mchezaji huyo atarejea kuichezea Simba kwa mkataba wa mwaka mmoja kwa mujibu wa makubaliano hayo.

Simba ilimuuza Okwi kwa dola 100,000 mwaka juzi Denmark, lakini kutokana na mchezaji huyo kutopata nafasi ya kucheza Ulaya, imeamua kumrejesha na makubaliano yamefikiwa Sh milioni 240.

“Dola 120,000 tu wale jamaa wanataka watuachie Okwi. Na Okwi naye atasaini kwa mshahara tu mkataba wa mwaka huu, hatumpi dau la kusaini yeye,”kimesema chanzo kutoka Simba.

Taarifa za mitandao ya kujamii jana zilieleza kuwa, Okwi ni mchezaji aliyeipa faida kubwa Simba ndani na nje ya uwanja wakati ule akiichezea klabu hiyo ya Msimbazi.

Mbali na kuwasaidia Wekundu hao wa Msimbazi kushinda matajii mbalimbali tangu ajiunge nao kwa mara ya kwanza mwaka 2010, mchezaji huyo pia aliinufaisha kifedha Simba.

Simba ilimuuza Okwi Etoile du Sahel ya Tunisia Januari mwaka 2013 kwa dau la rekodi kwa klabu za Tanzania, dola 300,000, ingawa baada ya muda akaingia kwenye mgogoro na klabu hiyo ya Tunisia. 

Mtafaruku ulianza baada ya Okwi kuchelewa kurejea mjini Sousse mkoani Sahel baada ya ruhusa ya kwenda kuichezea timu yake ya taifa, Uganda.

Okwi naye akadai Etoile walikuwa hawamlipi mishahara na kufungua kesi FIFA, ambayo mwisho wa siku alishinda kwa kuruhusiwa kutafuta timu nyingine ya kuchezea kulinda kipaji chake, wakati wa mgogoro wake na klabu ya Tunisia.

DOWNLOAD APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD BONYEZA HAPA  

ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: