![ads](http://1.bp.blogspot.com/-J5aEnGVep5k/WJTrf2fzuPI/AAAAAAAAU5U/_iuE-DY1RHAM5_hqPHb-UuNbabG2xn2nwCK4B/s1600/AdvertiseHere.jpg)
Profesa Ibrahim Lipumba Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF)
aliyefutwa uanachama na Baraza Kuu la Uongozi Taifa la Chama hicho,
amesema usaliti uliofanywa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(Chadema) kwa aliyekuwa Katibu Mkuu wake Dkt. Wilbroad Slaa na kukiuka
makubaliano ya Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) katika kipindi cha
kampenzi za uchaguzi mkuu wa 2015 utakigharimu chama hicho.
Lipumba ameyasema hayo Novemba 26, 2016 katika mkutano wake na
baadhi ya viongozi wa kata za Jimbo la Temeke kwenye Ukumbi wa Sunrise
ulioko Tandika jijini Dar es Salaam.
“Usaliti wa Chadema kwa Dkt. Slaa utaendelea kuigharimu na
ndio maana hawataki nirudi katika wadhifa wangu na nikirudi watakwisha,” amesema.
Amedai kuwa, usaliti wa Chadema umesababisha upinzani
kupokonywa ajenda yake ya ufisadi na kuruhusu Rais John Magufuli
kuitumia ajenda hiyo kumaliza nguvu ya upinzani.
“Rais Magufuli ametunyang’anya ajenda ya kusimamia ufisadi,
leo hii Chadema hawana ajenda ya kupinga ufisadi kwa sababu ya kumuasi
Slaa,” amesema.
Kuhusu Ukawa Lipumba amedai kuwa, baadhi ya viongozi wa Chadema
wanautumia umoja huo kuiua CUF Bara huku akituhumu baadhi ya viongozi
wa CUF kuwa wananjama za kukiuza chama hicho.
“Viongozi wanajua dhahiri athari za Ukawa na hata Julias
Mtatiro alipokuwa anagombea Ubunge Segerea alinitumia sms na sijaifuta
ipo, akisema kuwa kuna athari zitakazotukuta kuhusu mpango wa Chadema wa
kusimamisha wagombea katika majimbo ya CUF, leo hii anaungana nao,” amesema.
Aidha, amesema alifikia hatua ya kujiudhuru mwezi Agosti mwaka
jana uenyekiti wa CUF kwa madai ya kutokubaliana na hali ya kuwa mpiga
debe wa Edward Lowassa aliyekuwa mgombea wa kiti cha urais kwa tiketi ya
Chadema na mwamvuli wa Ukawa.
“Nilikataa kuwa mpigadebe wa Lowassa, niligombea urais mara
nne leo hii nisimame kumpigia debe Lowassa? Ambaye kwenye orodha ya
majina ya mafisadi jina lake lilikuwa namba nmoja. Nisingeweza fanya
hivyo nikaona bora kujiudhuru,” amesema.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI
Post A Comment: