![ads](http://1.bp.blogspot.com/-J5aEnGVep5k/WJTrf2fzuPI/AAAAAAAAU5U/_iuE-DY1RHAM5_hqPHb-UuNbabG2xn2nwCK4B/s1600/AdvertiseHere.jpg)
Siku tatu baada ya
kudaiwa kumfanyia fujo jirani yake, Mchungaji wa Kanisa la Maombezi
(GRC), Anthony Lusekelo maarufu Mzee wa Upako, amejibu tuhuma hizo
akisema anaishi kana kwamba hana jirani.
“...Tunaishi kama majambazi tu, hujui jirani yako ni nani,” amesema.
Lusekelo
amesema Yesu ambaye ni mwana wa Mungu alikubali kudhalilishwa na
baadaye kufa bila hatia hivyo na yeye alikubali kula kiapo katika nafasi
ya utumishi wake.
Amesema magazeti hayawezi kumshusha kwa kuwa hayakumpasha ila Mungu pekee.
Katika
mahubiri yake yaliyohudhuriwa na waumini wengi kama ilivyo kwa Jumapili
nyingine za karibuni kanisani kwake, Ubungo Kibangu, mchungaji huyo
aliingia kwa mapokezi ya wimbo wa kuabudu uitwao ‘Angalia Bwana’ kabla
ya waumini kuanza kumtunza kwa sadaka kama ilivyo kawaida ya ibada zake.
Alhamisi
iliyopita, mitandao ya kijamii ilikuwa na picha zinazomuonyesha Mzee wa
Upako akirushiana maneno makali na jirani yake lakini mchungaji huyo
hakupatikana kuzungumzia tukio hilo ambalo lilisambaa baada ya mwandishi
wa habari, Happiness Katabazi aliyeshuhudia mzozo huo, kuandika kwa
kirefu kisa hicho na kusambaza kwenye mitandao ya kijamii.
Picha
ya video iliyosambaa mitandaoni ilimuonyesha mtu anayedaiwa kuwa ni
mchungaji Lusekelo akijibizana na sauti ya mwanamke, ambaye haonekani,
huku gari la rangi nyeusi aina ya Toyota Landcruiser likiwa limeegeshwa
katikati ya barabara ya mtaani na kuzuia mengine kupita.
“Kwanza
waliandika habari kwamba waumini hawatakuja kanisani badala yake
wamejitokeza bila kukatishwa tamaa. Wakati mnajitokeza hapa mbele (kutoa
sadaka), alipita mama mmoja amebeba mtoto, nilimwombea mwaka jana hapa
kwamba atapata mtoto na leo amepata mtoto, sasa mbona magazeti
yasiandike habari hizo?”
“Kwa nini wasiandike hayo mazuri ‘front page’ (ukurasa wa mbele)?, halafu mnaandika Mzee wa Upako matatani, matatani babu yako.”
“Najua
na leo mmekuja mpo humu mnasubiri niseme, nasubiri mmalize kwanza
nyinyi halafu na mimi ndiyo nitasema, baada ya mwezi mmoja najua mtakuwa
mmemaliza,”amesema.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI
Post A Comment: