ads
 
Chapati ni aina ya mkate ambao hauumuliwi kw amira. Chapati hutayarishwa kwa unga wa ngano. hiki chakula ni kitamu sana na asili yake ni bara la Hindi

Mahitaji

Unga wa ngano kilo 1
 
Mayai 2
 
Chumvi
 
Maji
 
Siagi (butter) vijiko 3 vikubwa
 
Mafuta ya kula kwa ajili ya kuchomea
 
Iliki ya unga
 
Maziwa ya unga vijiko 3 vikubwa

Maelekezo


Weka unga kwenye beseni au sufuria kavu kisha weka chumvi kiasi, maziwa vijiko 3 vya chakula na hiriki.  Changanya mpaka uhakikishe vimechanganyikana vizuri.

Weka butter vijiko vitatu kwenye unga kisha changanya. Changanya hadi butter ishikane na unga vizuri na iwe na uwiano mzuri (isionekane kabisa).
 
Pasua mayai pembeni, yakoroge vizuri na kisha weka kwenye unga. Changanya zaidi hadi upate uwiano unaofaa.
 
Ukiona uwiano mzuri wa unga wako, weka maji ya uvuguvugu kwenye unga na anza kukanda. Kanda unga mpaka uwe laini na haushikani na chombo unachokandia wala haunati kwenye mikono. Hapo unga utakua tayari.
 
Kata mabonge ya unga kwa umbo la mviringo kisha weka kwenye chombo pembeni. Rudia hili zoezi hadi unga uishe.
 
Chukua donge mojamoja, paka unga weka kwenye kibao cha kusumia chapati. Sukuma chapati hadi iwe sawa. Paka mafuta kwenye chapati na anza kukunja.
 
Rudia hilo zoezi kwa madonge yote yaliyobaki. Ukimaliza, anza kusukuma chapati zako kwa ajili ya kupika.
 
Bandika kikaango jikoni. Acha kipate moto vizuri.
 
Weka chapati, acha iive hadi iwe rangi ya kahawia. Geuza upande wa pili, paka mafuta upande uliokua wa kahawia. Geuza, paka mafuta tena upande mwingine.
 
Hakikisha chapati inaiva vizuri na inachambuka,hapo utakua umemaliza kazi na tayari kula chapati zako.
 
DOWNLOAD APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD BONYEZA HAPA  

ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: