Jeshi la Polisi mkoani Mtwara limeuzuia mkutano wa uliotarajiwa kuhutubiwa leo na Katibu Mkuu wa CUF, Seif Sharif Hamad.
Mkutano
huo ulitegemewa kuanza saa 5 asubuhi lakini askari walionekana
wakizunguka geti la kuingia chuo cha Stella Maris (Stemmuco) ambako CUF
walitegemea kutumia ukumbi wao.
Katika
eneo la chuo hicho yalionekana magari matatu ya askari ambayo pia
yalikuwa yakizunguka katika mji wa Mtwara na gari moja la maji ya
kuwasha likiwa limesimama kando ya eneo la chuo hicho.
Mkurugenzi
wa habari, uenezi na uhusiano wa Umma CUF, Mbarala Maharagande amesema
mkutano huo ulilenga kukagua shughuli za chama, kupata maoni ya
wanachama pamoja na mapendekezo ya namna ya kuboresha utendaji wa chama
kwa ngazi za chini.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI



Post A Comment: