KOCHA Mkuu mpya wa Yanga, George Lwandamina amekanusha taarifa za
kuleta wachezaji kutoka Zesco lakini pia amekiri wachezaji wa Tanzania
ni legelege ukilinganisha na wale wa Zambia.
Lwandamina aliyasema hayo jana wakati akitambulishwa rasmi kwa
waandishi wa habari pamoja na Mkurugenzi wa Ufundi wa Yanga, Hans
Pluijm.
Lwandamina alisema hana mpango wa kubadilisha chochote kwenye benchi
la ufundi pamoja na wachezaji huku akikanusha kuwaleta nchini wachezaji
Jesse Were na Misheck Chaila, lakini akasema amekabidhiwa jukumu zito
ila analichukulia kama changamoto kuhakikisha Yanga inafanya vema.
“Nitapambana kuhakikisha Yanga inafanya vizuri, najua ni changamoto
mpya kwangu, lakini nitafanya kila linalowezekana kuhakikisha tunafanya
vizuri kuanzia kwenye ligi ya nyumbani hadi klabu Bingwa Afrika,”
alisema Lwandamina.
"Nasikia tetesi kuhusu wachezaji wapya kutoka Zesco kusajiliwa Yanga,
naomba ifahamike kuwa kama kocha mkuu sijui chochote labda mchakato huo
unafanyika bila mimi kushirikishwa, kwani kikosi kilichopo ndicho
nitaendelea nacho," alisema Lwandamina.
Pia Lwandamina alisema hakuna wachezaji aliowaleta japo amekiri
wachezaji wa Tanzania hawako fiziki kama wa Zambia kwani alishawaona
wakati wakicheza na Ruvu Shooting kwenye mechi ya mwisho ya mzunguko wa
kwanza wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara Akimzungumzia mtangulizi wake,
Lwandamina amemsifu Pluijm kwa kusema amefanya kazi nzuri na kuahidi
kufuata nyayo zake kwa kushirikiana naye bega kwa bega kuhakikisha Yanga
inapata mafanikio zaidi.
Mkurugenzi mpya wa ufundi, Pluijm alisema yeye hana shida na
kubadilishiwa majukumu kikubwa ataendelea kutimiza majukumu yake kwa
mujibu wa mkataba wake. Pluijm alianza kuifundisha Yanga 2014 na
ameiongoza katika mechi 128 kwenye awamu mbili, akishinda 80, sare 25 na
kufungwa 23.
Katika mechi 19 za nusu msimu mwaka 2014, alishinda 11, sare sita na
kufungwa mbili, wakati katika mechi 110 za tangu mwaka jana, alishinda
69, sare 19 na kufungwa 21.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI
Post A Comment: