ASKARI wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU),
Nassir Hassan Jecha, amefukuzwa kazi kwa tuhuma za kumfanyia mwanafunzi
mtihani wa kidato cha nne.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi, Nassor Ali Hassan, alisema
askari huyo alikamatwa katika chumba cha mtihani katika Shule ya
Sekondari ya Mwanakwerekwe A, akifanya mtihani wa somo la Kiswahili kwa
kutumia jina la Said Mwinyi Haji.
Alisema baada ya wasimamizi wa mtihani kumkamata askari huyo na
kubaini kuwa si mtahiniwa halali, Jeshi la Polisi lilifanya uchunguzi na
kubaini kuwa ni askari wao na alikuwa akimfanyia mtihani mtu mwengine.
“Jeshi la Polisi halipendi kuona linatiwa doa na kasoro kwa kuwa lina
dhamana kubwa kwa taifa, hivyo tunapogunduwa kosa lolote lazima tufanye
uchunguzi na likimhusisha askari wetu ni lazima kumchukulia hatua
zinazostahili,”alisema.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI



Post A Comment: