Kiungo mshambuliaji Georginio Gregion Emile Wijnaldum yupo shakani
kucheza mchezo wa mwanzoni mwa juma lijalo ambapo klabu yake ya
Liverpool itakua mwenyeji wa Man Utd katika uwanja wa Anfiled.
Wijnaldum ameibua hofu ya kuukosa mchezo huo unaosubiriwa kwa hamu
kubwa na mashabiki wengu duniani, kufuatia majeraha aliyoyapata wakati
wa mchezo wa kuwania kucheza fainali za kombe la dunia kati ya timu yake
ya taifa ya Uholanzi dhidi ya Ufaransa uliochezwa usiku wa kuamkia hii
leo mjini Amsterdam.
Kiungo huyo ambaye alisajiliwa na Liverpool akitokea Newcastle miezi
mitatu iliyopita, alilazimika kutolewa uwanjani, baada ya kulalamika
anahisi maumivu makali sehemu za nyuma ya paja.
Tayari meneja wa Liverpool Jurgen Klopp ameagiza mchezaji huyo
kufanyiwa vipimo ili kufahamu kama atakuwa na uwezo wa kumchezesha
katika mchezo ujao wa ligi kuu ya soka nchini Uingereza dhidi ya Man
Utd.
Tangu aliposajiliwa huko Anfield, Wijnaldum ameshacheza michezo 11,
na kabla ya kujiunga na timu yake ya taifa alikua sehemu ya kikosi cha
Liverpool kilichoibuka na ushindi wa mabao mawili kwa moja dhidi ya
Swansea City.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI
Post A Comment: