MWENYEKITI wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Joseph Butiku amepongeza ukaguzi wa vyeti pamoja na mfumo wa uchumi, unaofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano ya Rais John Magufuli.


Alisema kuwa ni hatua nzuri ya kurejesha nidhamu na maendeleo ya nchi na kuwataka wananchi kumuunga mkono na sio kulalamika.

Butiku alisema hayo juzi kwenye mazungumzo maalumu na gazeti hili, ambapo alisema kuwa kinachoendelea kwa sasa ni utekelezaji wa sheria na kanuni ambazo awali zilichezewa.

Alisema kushindwa kufuatwa kwa taratibu kulitengeneza mianya mbalimbali kwa wananchi kujiamulia mambo yao, huku wengine wakiichezea elimu ambayo ndio msingi wa taifa.

Butiku alionesha kukerwa zaidi na utitiri wa vyeti vya kufoji, uliokuwa umekithiri serikalini na kuipongeza serikali kwa uamuzi wake wa kukabiliana na hali hiyo sasa, kwa kufanya uhakiki wa vyeti vya watumishi wa umma.

Alisema kuwa inashangaza kuona kuwa kuna watu walikuwa wamefikia hadi hatua ya kuwa na vyeti vya juu vya Shahada ya Uzamili (Masters) na Uzamivu (PHD), lakini vya kidato cha nne hawana.

β€œKile kinachoendelea kwa sasa ni utekelezaji wa ahadi ya kurejesha mifumo ya nidhamu kwenye serikali, sasa kinachotakiwa ni kuunga mkono kwa kuhakikisha kuwa malengo ya Rais yanatimia kwa sasa,” alisema Butiku.

Hivi Karibuni Butiku akizungumza na Gazeti Moja la kila Siku alinukuliwa akisema kuwa Chama Chake cha CCM kimekithiri kwa Rushwa hali aliyosema kuwa ni kinyume na miiko na matakwa ya katiba ya chama hiko.

DOWNLOAD APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD BONYEZA HAPA  

ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: