ads

Sniper ni specialists/wataalamu wanaohusika na ulengaji shabaha mahiri sana wanaotumia silaha maalumu. Snipers hutimiza misheni zao aidha wakiwa peke yao yaani "one man army" au wakiwa katika pair.


Sniper hutumia silaha kali, zenye umakini na zenye kiona mbali kikali ili kuhakikisha jicho lake liko karibu na adui. Sniper huwa na mazoezi makini, makali na ya kurudia rudia ili kuhakikisha anakuwa mlengaji mahiri na asiyekosea.

Mara kadhaa Sniper huwa na mawasiliano complex na unit yake anayoitumikia ili kutoa taarifa makini kwa wenzake japo wengi wa Sniper hufanya kazi zao peke yao.

Sniper
mara nyingi hupitia mazoezi magumu, makini na imara ili kuwa bora na mara nyingi Snipers huwa ni wagunduzi wa maeneo yasiyoonwa na wengine. Hufunzwa namna nzuri ya kulenga shabaha fupi na ndefu wakitumia riffles zenye vipimo na utimilifu halisi.

Snipers huweza kuhama eneo kwa haraka na bila kugundulika baada ya kuachia risasi na kumu-eliminate adui. Mara nyingi Sniper huvaa mavazi au sura zinazoendana na mazingira kama kinyonga ili kuepuka kuonekana na adui.
Sniper hutumia akili zaidi na ufanisi kuliko nguvu. Pia hupata mafunzo ya kichunguzi, kimapambano, utii na kutunza siri endapo kwa bahati mbaya atatekwa na adui.

Viongozi wengi duniani huwatumia walinzi hawa Snipers ili kuwa salama.


DOWNLOAD APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD BONYEZA HAPA  

ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: