ads

Mshambuliaji wa timu ya Simba anayeongoza kwa kufunga magoli 7 katika mechi 9 alizocheza ligi kuu Tanzania bara msimu huu Shiza Kichuya amesema kila atakapo pata nafasi kazi yake ni kufunga.


Kichuya ameyasema hayo katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es salaam baada ya kumalizika kwa mchezso kati ya Simba na Kagera Sugar mtanange ambao umemalizika kwa Simba kuibuka kidedea kwa kuicharaza Kagera Sugara bakoran 2 kwa bila.

“Wachezaji kazi yetu ni kufunga, na mimi kila nitakapopata nafasi kazi ni kufunga na lengo letu ni kuendelea kuwa wamoja kama ilivyo sasa ambapo mashabiki pamoja na viongozi na wachezaji tupo wamoja ndiyo maana hata matokeo yanaonekana” Amesema Kichuya

Wakati huo huo Nahodha wa Kagera Sugar George Kavila amesema Simba imepata nafasi na kuzitumia vizuri ndiyo maana wakaweza kuibuka na ushindi huo

“Ligi hii ni ngumu huwezi kusema wameshinda kwa bahati, wamepata nafasi wakazitumia tutaenda kujipanga vizuri kwa michezo inayofuata” Amesema Kavila.

DOWNLOAD APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD BONYEZA HAPA  

ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: