Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed
Shein (kulia)akipokea mmoja wa Miongoni mwa Misahafu elfu kumi
iliyotolewa na Mfalme wa Morocco, Mohammed VI,mara baada ya Swala ya
Ijumaa iliyoswaliwa leo katika Msikiti wa Mwembeshauri Mjini
Unguja,Mfalme Mohammed VI akiwa katika ziara ya kibinafsi na ujumbe
wake, ambapo amefikia katika Park Hyatt Hotel- Shangani Mjimkongwe wa
Zanzibar,[Picha na Ikulu.]28/10/2016.
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed
Shein na Mfalme wa Morocco, Mohammed VI, (katikati) pamoja na Viongozi
mbali mbali na Ujumbe wa Mfalme wakijumuika na Waislamu wengine
wakiswali swala ya Ijumaa iliyoswalishwa na Sheikh Fadhil Soraga katika
Msikiti wa Mwembeshauri Mjini Unguja,Mfalme Mohammed VI yupo Nchini
kwa ziara ya kibinafsi
Mfalme
wa Morocco, Mohammed VI(kulia) akisalimiana na Katibu wa Mufti wa
Zanzibar Sheikh Fadhil Soraga mara baada ya kuswalisha Swala ya Ijumaa
katika Msikiti wa Mwembeshauri Mjini Unguja,Mfalme Mohammed VI yupo
Nchini kwa ziara ya kibinafsi
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed
Shein (kushoto) akifuatana na Mfalme wa Morocco, Mohammed VI, pamoja na
Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe,Ayoub Mohamed Mahmoud (kulia)
wakitoka nje ya Msikiti wa Mwembeshauri Mjini Unguja baada ya swala ya
Ijumaa leo
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed
Shein (kushoto) akiagana na Mfalme wa Morocco, Mohammed VI, mara baada
ya kumalizika kwa swala ya Ijumaa leo katika Msikiti wa Mwembeshauri
Mjini Unguja,Mfalme wa Morocco, Mohammed VI yupo nchini na ujumbe wake
kwa ziara ya kibinafsi Zanzibar.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI
Post A Comment: