Mchakato unaofanywa
na klabu ya Yanga wa kutaka kukodisha nembo na timu hiyo kwa mwenyekiti
wao, Yusuf Manji unakwenda kinyume na Katiba ya klabu hiyo kongwe
nchini.
Katiba
ya Yanga ya 2010 inayotambuliwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na
Baraza la Michezo Tanzania (BMT), ibara ya 56, ibara ya 56, ibara ya 56
inatambua suala la klabu hiyo kubadilika kuwa kampuni ya umma na siyo
mali ya mtu mmoja au kikundi.
Ibara
ya 56 yenye kichwa cha habari, Kampuni ya Umma ya Yanga inaonyesha
jinsi klabu hiyo itakavyofuata utaratibu wa kubadilika na kuingia katika
mfumo wa kampuni.
Ibara
ya 56 (1), inaeleza kuwa kutakuwa na kampuni itakayojulikana kama Young
Africans Corporation Limited itakayosajiliwa chini ya Sheria ya
Makampuni ikiwa kampuni ya umma yenye hisa.
Ibara
ya 56(2), “Wanachama wote ambao katika tarehe ya marekebisho ya katiba
ya mwaka 2007 wako hai, watakuwa, kwa nguvu ya uanachama wao, wanahisa
katika kampuni kwa kiwango cha idadi ya hisa watakazopata kwa mujibu wa
mwafaka wa Yanga uliofikiwa Juni 6, 2006.
Ibara
ya 56 (3) inasema, “Klabu itamiliki hisa zilizo sawa na asilimia
hamsini na moja (51) ya hisa zote zilizopo katika kampuni.
Ibara ya
56 (4) inasema,” Mkutano mkuu wa uchaguzi utachagua wanachama wawili
ambao siyo miongoni mwa viongozi wa klabu kuwa wajumbe wa bodi ya
wakurungenzi wa kampuni kwa ajili ya kuwakilisha masilahi ya klabu
kwenye kampuni.
Hivyo,
uamuzi wa Manji kuanzisha kampuni, Yanga Yetu Limited anayoimiliki kwa
asilimia 99 na kukodisha timu na nembo ya klabu hiyo kwa kipindi cha
miaka kumi unapingana na Ibara 56 (3) inayotoa nafasi kwa klabu kumiliki
asilimia 51 za hisa.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI



Post A Comment: