MWENYEKITI wa Yanga, Yusuf Manji, amesitisha kuendelea na zoezi la kuikodisha timu na nembo ya klabu hiyo na kuwaambia wasaidizi wake, wasitishe mipango yote ya maendeleo waliyokuwa wameanza kuifanya.


Manji amewaambia wasaidizi wake kusitisha maandalizi ya Ligi ya Vijana ya Matawi ya Yanga, lakini amewaambia waandae siku rasmi ambayo atazungumza na vyombo vya habari na kuwaomba radhi Wanayanga ambao wamemuunga mkono muda wote.

Habari za uhakika ambazo Championi Jumatano limezipata, zinasema Manji alizungumza na wasaidizi wake jana mchana ikiwa ni dakika chache baada ya TFF kufanya mkutano na waandishi wa habari na kusema hawatambui suala la Yanga kuikodisha timu na nembo kwa Kampuni ya Yanga Yetu Ltd, kwa miaka 10.

“Leo alionekana ni kama mtu aliyekata tamaa au asiyefurahishwa na jambo. Amewaita wasaidizi wake na wamefanya kikao, hakikuwa kirefu sana.

“Amewaambia ameamua kuachana na masuala ya kuikodisha Yanga, pia amesema ameona ni vizuri kuachana na masuala ya mpira.

“Kilichomuudhi ni wale wasiotaka mchakato wa mabadiliko Yanga, lakini hawatoi hoja za msingi,” kilieleza chanzo.

“Wasaidizi wake walikuwa wameanza mchakato wa kutengeneza mfumo wa Ligi ya Vijana ya Matawi ambao ungeigharimu Yanga yetu takribani Sh milioni 280 kwa ajili ya vifaa, uendeshaji na kadhalika.“Lakini kuna suala amelizungumzia la uchaguzi, hilo sijaelezwa vizuri. Huenda Yanga wakaitisha uchaguzi tena ili kuchagua viongozi yeye atakapotangaza kujiuzulu rasmi. 

“Anaweza kufanya hivyo, yaani kutangaza kujiuzulu na kutangaza uchaguzi, pia kuwaomba radhi wanachama na mashabiki waliomuunga mkono muda wote.”

CREDIT- CHAMPION

DOWNLOAD APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD BONYEZA HAPA  

ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: