Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimesema ni uongo na ni
propaganda za wapinzani wao kwamba Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa
alimhonga Mwenyekiti Freeman Mbowe ili kupata nafasi ya
kugombea urais mwaka 2015.
Hayo yamesemwa na katibu Mkuu wa chama hiko Dk Vicent Mashinji wakatia lipokuwa akifanya mahojiano ya moja kwa moja na wananchi kupotia ukurasa wa kijamii wa Facebook.
“Si kweli kwamba Mwenyekiti Freeman Mbowe alimhonga Lowassa ili
agombee urais kupitia CHADEMA , ni propaganda zinazoenezwa na wapinzani
wetu ili kuwadanganya wananchi” Amesema Dkt. Mashinji.
Amesema Lowassa alijiunga na CHADEMA kwa njia halali kwa mujibu wa
taratibu za chama, na maamuzi ya kumteua kugombea urais yalifanywa na
vikao halali kuanzia ngazi ya Kamati Kuu hadi Mkutano Mkuu.
Kuhusu sababu za CHADEMA kumkaribisha Lowassa licha ya kumtaja miaka
mingi kuwa alihusika na ufisadi, Dkt Mashinji, hakutaka kulifafanua kwa
undani, lakini aliishia kusema kuwa wao walijiridhisha kuwa hakuwa na
hatia yoyote na kwamba kama kweli alikuwa ni fisadi, basi vyombo vya
dola vingemchukulia hatua.
"Kama mtu kweli alikuwa ni fisadi, kwanini hakuwahi kuchukuliwa
hatua, hata kufikishwa mahakamani?, nadhani hilo tuliache" Alisema kwa
ufupi Dkt Mashinji.
Aidha Dkt. Mashinji amewataka watanzania na wapenzi wa CHADEMA
kufahamu kwamba chama hicho hakipo kimya bali kinaendelea na mikakati ya
kuhakikisha kwamba kinawafikia watanzania kwa kuwatetea kwa kila hali
kutokana na mambo yanayoendelea nchini.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI
Post A Comment: