ads

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimemkingia kifua aliyekuwa Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) Edward Lowassa kwa kusema mchakato wa kumpata ulizingatia demokrasia na matakwa ya katiba za vyama.


Aidha, kimeeleza kuwa Lowassa ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, alipita hatua zote kama mwanachama halali wa Chadema mwenye haki sawa na mwanachama mwingine yeyote, kwa mujibu wa kifungu cha 5.1 cha Katiba yao.

Hayo yalielezwa na Mkuu wa Idara ya Uenezi ya Chadema, Hemedi Ali wakati akizungumza na waandishi wa habari katika Makao Makuu ya chama hicho kuhusu tuhuma zilizotolewa na Msemaji wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Christopher ole Sendeka.

Ali alisema, mchakato wa kumpata mgombea Urais na Mgombea Mwenza wa chama hicho ulikuwa wa kidemokrasia kwa mujibu wa Katiba yao ambayo Ibara ya 7.7.16 (a), Kamati Kuu imepewa mamlaka ya kuwafanyia utafiti wagombea urais wa chama hicho na kupeleka ripoti katika Baraza Kuu ambalo linapendekeza majina kwa mujibu wa Katiba na Mkutano Mkuu utachagua mgombea.

“Ni kawaida ya CCM kuchafua mtu ambaye atakuwa na msimamo na nia ya kulivusha Taifa, wamefanya hivyo kwa viongozi wetu wa chama na watu binafsi hivyo hatushangai walivyomshambulia Lowassa akiwa ndani ya CCM na sasa Chadema,” alisema Ali.

Alisema kumekuwa na tuhuma kuwa yupo kiongozi ndani ya chama hicho, aliyepata dola za Marekani milioni 15 ambazo ni takribani Sh bilioni 33 ili apange safu ya uongozi ndani ya Chadema, jambo ambalo si la kweli.

Jana CCM kupitia Msemaji wake, walimtaka Lowassa kutafakari dhana pana ya demokrasia iliyopo nchini kabla ya kumshutumu Rais John Magufuli kwamba anakiuka misingi yake.

DOWNLOAD APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD BONYEZA HAPA  

ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: