![ads](http://1.bp.blogspot.com/-J5aEnGVep5k/WJTrf2fzuPI/AAAAAAAAU5U/_iuE-DY1RHAM5_hqPHb-UuNbabG2xn2nwCK4B/s1600/AdvertiseHere.jpg)
HARAKATI za aliyekuwa Mwenyekiti wa Taifa wa
Chama cha Wananchi (Cuf), Profesa Ibrahim Lipumba kutaka kuwania tena
kiti hicho, zimeanza rasmi baada ya kiongozi huyo kuibuka katika msiba
wa Ismail Mapande 'Kundambanda' na kuonyesha alikusudia kupiga kampeni.
Prof.Lipumba ambaye aliachia ngazi nafasi hiyo wakati Cuf ikijiandaa
na Uchaguzi Mkuu wa Desemba 25 mwaka jana, aliibuka ghafla msibani na
kutengeneza fursa kadhaa za kuzungumza na waombolezaji kabla na baada ya
Kundambanda aliyekuwa mgombea wa ubunge jimbo la Masasi kupitia Cuf
kuzikwa.
Kwanza alitambulishwa kuwa mgeni rasmi, wakati aliyepewa nafasi hiyo
ni Mkurugenzi wa Sera na Uchaguzi wa Cuf Taifa, Shaweji Mketto ambaye
licha ya kuwapo kwake katika tukio, ugeni rasmi ukaelekezwa kwa
Prof.Lipumba.
Akuzungumza katika msiba huo, Prof.Lipumba alikiri kuwa licha ya
kufanyakazi kwa kipindi kifupi na marehemu Kundambanda, ilitosha
kutambua uwezo na ushawishi mkubwa aliokuwa nao kisiasa.
Mwenyekiti huyo mstaafu alitoa sh.50,000 na kuahidi nyingine 150,000
ili zitumike kufungua akaunti maalum ya mtoto wa miaka mitano wa
marehemu Kundambanda ili zimsaidie katika elimu mara atakapoanza elimu
ya sekondari.
Hata hivyo, wakizungumza katika tukio hilo baadhi ya waombolezaji na wengi wao wakiwa wafuasi wa chama cha Cuf na Chadema, walisema hatua hiyo ya Prof.Lipumba ni mpango wake wa kuanza
kushawishi wanachama ili wampigie kura wakati wa uchaguzi unaotarajiwa
kufanyika Agosti 21 mwaka huu,
Muombolezaji Issa Matandu amesema kuwa Prof.Lipumba hafai tena
kuchaguliwa kuwa mwenyekiri wa Cuf kwa sababu alikiteleza chama wakati
mgumu na dhamira yake ililenga kuona chama kinakufa kabisa.
credit- Nipashe
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI
Post A Comment: