SHIRIKISHO la wamiliki na mameneja wa shule na vyuo visivyo vya
kiserikali Tanzania (TAMONGSCO) limesema ipo haja kwa serikali kutangaza
ada elekezi mapema ili kuondoa utata uliopo unaotishia kukwamisha
maendeleo ya elimu.
Shirikisho hilo limesema kwamba mambo mengi ya maendeleo katika shule hizo yamekwama kutokana na kusubiri ada elekezi.
Akizungumza kumkaribisha Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia,
Profesa Joyce Ndalichako, katika mkutano wa shirikisho hilo mjini hapa,
Mwenyekiti wa Shirikisho Mrinde Mzava, alisema walifurahishwa na kufika
kwake Waziri, kwani waliamini kupata maelekezo ya ada elekezi ili
kumaliza shida zilizopo sasa za uendeshaji.
Alisema mwenyekiti huyo kwamba kuna hatari katika elimu kama hali ya
ucheleweshaji wa uchambuzi wa gharama za ada elekezi itaendelea.
Alisema pamoja na serikali kukiri kuwa suala hilo lip
o mezani kwa
ajili ya mazungumzo, hivi sasa shule na vyuo binafsi vimejikuta vikiweka
viwango visivyotakiwa kisheria ambapo kwa upande wao kuna madhara
makubwa.
Mwenyekiti huyo alisema kutokana na suala la ada elekezi kuwa kwenye
mazungumzo wanaiomba serikali iliangalie kwa haraka ili lipunguze mzigo
wa gharama za uendeshaji na ukubwa wa ada kwa lengo la kufanikisha
utoaji wa elimu bora.
Katika mkutano huo serikali imeelezea kusikitishwa kwake na baadhi ya
shule na vyuo kugeuza elimu kama sehemu ya kufanyia biashara. Aidha
imesema kuwa bado haijapitisha ada elekezi kwa wamiliki wa shule na vyuo
vya watu binafsi kutokana na jambo hilo kuwa kwenye meza ya mazungumzo
kati serikali na wamiliki hao.
Kauli hiyo ambayo imetolewa na Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia
na Mafunzo ya Ufundi, Prof Joyce Ndalichako, wakati wa ufunguzi wa
mkutano mkuu wa mwaka wa shirikisho la wamiliki na mameneja wa shule na
vyuo visivyo vya kiserikali Tanzania (TAMOMGSCO) mjini Dodoma.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
Post A Comment: