RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Ali Mohamed
Shein, amesisitiza haja ya kuimarisha zaidi uhusiano na ushirikiano
uliopo kati ya Tanzania na Japan.
Alisema hiyo inatokana na taifa hilo kutambua hatua za nchi hiyo za
kuendelea kuiunga mkono Tanzania katika kuimarisha miradi mbalimbali ya
maendeleo.
Dk Shein alisema hayo jana Ikulu mjini Zanzibar, wakati alipozungumza na Balozi mpya wa Tanzania nchini Japan, Mathias Chikawe.
Katika mazungumzo hayo Dk Shein alimueleza Balozi huyo kuwa Tanzania
ikiwemo Zanzibar, inajivunia uhusiano na ushirikiano mzuri pamoja na
hatua za Japan za kuendelea kuiunga mkono katika kukamilisha miradi
kadhaa ya maendeleo hapa nchini.
Alisema Serikali ya Japan pamoja na Shirika lake la Maendeleo la
Jica, kwa muda mrefu zimekuwa zikiunga mkono uimarishaji wa miradi ya
maendeleo hapa nchini, ambapo kwa upande wa Zanzibar nchi hiyo imesaidia
mradi mkubwa wa maji katika Mkoa wa Mjini Magharibi, ambao hivi sasa
upo katika awamu ya tatu.
Dk Shein pia alitumia fursa hiyo kumueleza Balozi huyo kuwa ipo haja
ya kuitangaza zaidi Tanzania kiutalii kutokana na kuweko vivutio kadhaa
kama fukwe nzuri za bahari kwa Zanzibar na hifadhi za Taifa kwa Tanzania
Bara.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
Post A Comment: