ads

MOISE Katumbi Gavana wa zamani wa jimbo la Katanga, Mkurugenzi wa klabu ya TP Mazembe na mfanyabiashara marufu nchini Kongo ametangaza kugombe urais wa Novemba mwaka huu,


Muungano wa vyama kadha vya upinzani umemuidhinisha Katumbi kuwa mgombea huku muungano huo huku ukiwa wamegubikwa na hofu ya huenda Rais Joseph Kabila akaendelea kushikiri madaraka kinyume na katiba hiyo.

Katumbi amekuwa Gavana wa jimbo la Katanga tangu 2007 chini ya chama cha People’s Party for Reconstruction and Democracy(PPRD) na baadae akajiuzulu nafasi hiyo septemba 2015 ambapo mwaka hu 2016 amekuwa akitoa kauli zinazo mtaka Kabila kuheshimu katiba ya taifahilo inayo mtaka kustaafu mwishoni mwamwaka huu.

Licha ya Katumbi kumsaidia Kabila katika kampeni uchaguzi wa mwaka 2006 na 2011 kwasasa anaonekana kuwa mbali na kiongozi huyo tangu kujiuzulu kwake 2015.

Hata hivyo mfanyabiashara amekuwa na umaarufu mkubwa kutokana kumiliki klabu ya TP Mazembe tangu 1997.

Uchaguzi huo unaonekana kuwa na mchuano mkali kwa kuwa Katumbi ana nguvu kubwa ya kiushindani kuanzia katika jimbo la katanga na katika ngazi ya taifa licha ya kukabiliwa na tuhuma za ubadhilifu wakati wauongozi wake.

Wachunguzi wa habari za siasa wamesema nchi hiyo inanyemelewa na machafuko iwapo Rais Kabila atataka kuendelea kuongoza taifa hilo kwa nguvu kama ilivyo fanyika Burundi na Rais Nkurunzinza.



DOWNLOAD APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD BONYEZA HAPA
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: