Shirikisho la soka barani Ulaya UEFA, limemtangaza mwamuzi kutoka
nchini England, Mark Clattenburg kuwa msimamizi mkuu wa dakika 90 za
mchezo wa hatua ya fainali ya ligi ya mabingwa barani humo, ambao
utashuhudia Real Madrid wakipapatuana na Atletico Madrid Mei 28 mjini
Milan nchini Italia.
Clattenburg mwenye umri wa miaka 41, ametangazwa na kupewa jukumu
hilo, kutokana na hatua ya kuonyesha kiwango kizuri cha uchezeshaji kwa
msimu huu, na inaaminiwa atatoa haki katika mchezo huo unaosubiriwa kwa
hamu kubwa na mashabiki wote wa soka duniani.
UEFA pia wamemtangaza mwamuzi kutoka nchini Sweden, Jonas Erksson
mwenye umri wa miaka 42, kupuliza filimbi katika mchezo wa hatua ya
fainal ya Europa League.
Mchezo huo utashuhudiwa majogoo wa jiji Liverpool wakipambana na
mabingwa watetezi Sevilla CF kutoka nchini Hispania, Mei 18 katika
uwanja wa St Jacob Park uliopo mjini Basel nchini Uswiz.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
Post A Comment: