Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa DSM ikiongozwa na Mkuu wa Mkoa
wa DSM Paul Mkonda wamegundua Sukari iliyofichwa katika jengo la
ghorofa tisa ambalo liko katika jengo linalojengwa lililopo katika eneo
la Hananasifu -Kinondoni huku mmiliki wa sukari hiyo Bw,Bashir Ismail
mwenye asili ya kiasia akitiwa mbaroni na jeshi la Polisi.
Sukari hilo inadaiwa kuingizwa usiku katika jengo hilo huku kikiwa
katika mifuko ya viroba vya kilo 25,na ishiri lakini pia ikifungwa
katika mifuko midogo ya Plastiki ya kilo moja moja.
Mkuu wa Mkoa wa dsm Paul Makonda akizungumza na waandishi wa habari
amesema baadhi ya wafanyabiashara wameendelea kukaidi agizo la serikali
kwa kuficha sukari katika maghara na maeneo mbali mbali na kuahidi kuwa
Oeresheni dhidi ya wafanyabiashara hao ni ya kudumu.
Bw, Bashir Ismail ambaye alikuwa chini ya Ulinzi wa jeshi la Polisi
alihojiwa na kudai sukari hiyo iliyohifadhiwa katika jengo hilo
inapelekwa katika vituo vya kijamii ingawa alishindwa kujieleza jinsi
mazingira iliyowekwa huku ikifanyika kazi ya kuweka katika viroba kwa
kuwa eneo hilo linafanyika ujenzi na sio kiwandani.
Aidha Mkuu wa mkoa amewaonya wafanyabiashara wa Mkoa wa dsm kuwa
wamebaini kuwapo njama za kuficha bidhaa nyingine ikiwemo mchele na
mafuta katika kipindi hiki kuelekea mfungo wa ramadhani na kutoa onyo
lifuatalo.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
Post A Comment: