ads

Serikali imesema kupitia wadau mbalimbali wameanzisha programu maalum ya kuwawezesha vijana kujikwamua kiuchumi kwa kuweza kuwasaidia kupata fursa ya mitaji na mikopo ili kufanya shughuli mbalimbali za kujiingizia kipato


Akizungumza  mjini Dodoma, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Walemavu, Antony Mavunde amesema lengo la kufanya hivyo ni kuweza kuwatoa vijana kushinda vijiweni bila ya kazi maalumu huku wakilalamikia ukosefu wa ajira.

Mhe. Mavunde amesema kuwa kupitia Baraza la Kuwawezesha Wananchi Kiuchumi,(NEEC), Shirila la Kazi Duniani (ILO), Plan International ambao wanatoa misaada kwa vijana wasomi na wafanyabishara kwa kuwapa mitaji na mafunzo ya kufanya shughuli mbalimbali za kujiingizia kipato.

Aidha, Naibu Waziri huyo amesema kuwa tayari wakuu wa mikoa wameshaambiwa washirikiane na halmashauri zao kwa kutenga eneo maalumu ya kiuchumi kwa ajili ya vijana ili ya kuwawezesha vijana kupata fursa ya kushiriki katika kuinua uchumi wa nchi yao.

Mhe. Mavunde amesema kuwa vijana wengi wapo tayari kwa ajili ya kujiajiri lakini wanakumbana na changamoto ya mitaji pamoja na ukosefu wa kufanya shughuli hizo hivyo serikali imeamua kuchukua jukumu la kuwawezesha ili kujikwamua kiuchumi.

DOWNLOAD APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD BONYEZA HAPA
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: