POLISI mkoani Rukwa inawashikilia askari wake wawili wa Kituo Kikuu
cha Polisi wilayani Nkasi, wakituhumiwa kuomba na kupokea rushwa ya
zaidi ya Sh milioni 7.2 wamsaidie mtuhumiwa.
Kaimu Kamanda wa Polisi wa Rukwa, Leonce Rwegasira alitaja askari hao
kuwa ni Konstebo Filbert Ruhemeja na Konstebo Bahati Sengerema, ambao
walikuwa wakifanya kazi katika Kituo cha Polisi mjini Namanyere wilayani
Nkasi.
Alisema polisi inawafanyia uchunguzi wa kina askari wake wawili,
wanaotuhumiwa kwa kashfa ya kuomba rushwa ya Sh milioni 7.2 na iwapo
watabainika halitasita kuwatimua na kuwafikisha mahakamani.
Alisema askari hao wawili wa polisi, wanatuhumiwa kuomba na kupokea
rushwa ya fedha kutoka kwa mtu mmoja (jina linahifadhiwa) ili wamsaidie
katika shitaka linalomkabili.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
Post A Comment: