MBUNGE wa Viti Maalumu, Angelina Malembeka (CCM) ametaka watu
wanaohukumiwa kifungo cha maisha jela kwa kosa la ubakaji na ulawiti,
wahasiwe ili wawapo gerezani wasiendeleze tabia hizo.
“Tumeshaona wanaohukumiwa kifungo cha maisha, wakiwa huko gerezani
wanaendeleza vitendo vya kulawitiana, kwa nini sasa wasihasiwe?”
Alihoji. Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Harrison Mwakyembe, wakati
akimjibu jana alisema, “siwezi kuwa na jibu kwa sababu Bunge ndilo
linalotunga sheria, mbunge aje na wazo lake hapa bungeni lipitishwe kama
sheria sisi Serikali hatuwezi.”
Akitoa ufafanuzi zaidi juu ya hali ya ubakaji na ulawiti, Dk
Mwakyembe alisema kila siku nchini kunaripotiwa matukio 19 ya kubakwa na
kulawitiwa.
Alisema hali ni mbaya sana na sasa kuna mashauri 2,031 yaliyoripotiwa
mahakamani katika kipindi cha Januari hadi Machi mwaka huu. Kati yake
mashauri hayo, 111 yameshakamilishwa kwa kuhukumiwa ambapo watu 99
wamefungwa, watuhumiwa 18 wameachiwa huru kwa kukosa ushahidi na kesi
1,920 hazijakamilika.
Akijibu swali la msingi la mbunge huyo aliyehoji mpango wa Serikali
kuhakikisha kesi za kubakwa na kulawitiwa hazimalizwi kifamilia, Dk
Mwakyembe alisema kumalizwa kwa kesi kifamilia kunachochea vitendo hivyo
kuendelea katika jamii.
“Tatizo la kuficha ushahidi na kumaliza kesi hizo kifamilia, haliwezi
kumalizwa na vyombo vya dola peke yake bila ushirikiano na wananchi
wanaoishi na watuhumiwa. Hivyo Serikali imekuwa ikitoa elimu kwa umma
kuwa kuficha ushahidi na kuyamaliza matukio hayo ya jinai kifamilia si
kosa peke yake, bali vilevile utaratibu huo unachochea vitendo hivyo
kuendelea katika jamii,” alifafanua.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
Post A Comment: