ads

Uhaba wa wataalamu wa Afya wilayani Mbozi mkoani Songwe umesababisha wakazi wa kijiji cha Itepula kata ya Igamba wilayani humo kukosa huduma za matibabu kwa miezi mitatu sasa kufuatia muuguzi katika Zahanati ya kijiji chao kwenda likizo ya uzazi.


Wakazi wa kijiji cha Itepula wamebainisha hayo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kijijini hapo ukiwakutanisha na madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Mbozi walioongozwa na mwenyekiti wao Eliki Ambakisye.

Mmoja wa wakazi hao Bibi Sikudhani Mkondya amesema suala la kufungwa kwa zahanati kutokana na kukosekana muuguzi limekuwa kero kwao kwasababu miezi mitatu imepita sasa na wanalazimika kutembea umbali mrefu kufuata huduma za matibabu katika vijiji vingine.

Bi Mkondya pia amesema kufuatia kukosekana kwa mtaalamu kijijini hapo baadhi ya wakazi wanalazimika kutumia dawa pasipo ushauri wa kitabibu hivyo kubaki wakimeza dawa kwa kukisia hata kama hawajui ugonjwa unaowasumbua.

Afisa mtendaji wa kijiji cha Itepula Bwana Timothy Msukwa alikiri zahanati ya kijiji hicho kufungwa tangu Januari mwaka huu hivyo wananchi kuhangaika kupata matibabu kwani walizoea kupata huduma jirani.
Bw. Msukwa amesema chanzo cha kufungwa kwa zahanati hiyo ni baada ya muuguzi aliyekuwa anatoa huduma katika zahanati hiyo kwenda likizo lakini akabainisha kuwa tayari wamempata muuguzi mwingine ambaye tayari ameripoti lakini hajaanza kufanya kazi.

Kwa upande wake mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Mbozi Erick Ambakisye ameagiza zahanati kufunguliwa mara moja huku akimtaka muuguzi aliyepangiwa kituo hicho kufika mara moja na kuanza kazi ili kutoa hudumia wananchi.
DOWNLOAD APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD BONYEZA HAPA

ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: