Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa amesema
bungeni leo wakati akifanya majumuisho ya bajeti yake kuwa, Serikali
imeagiza sukari nje ya nchi kuukabili uhaba wa bidhaa hiyo.
Amewaagiza maofisa biashara wa wilaya, mikoa na Taifa kukagua maghala yote ya wafanyabiashara walioficha sukari na kuwachukulia hatua.
Waziri Majaliwa alisema hayo leo asubuhi wakati akihitimisha mjadala wa hotuba ya mapato na matumizi ya ofisi yake na kuliomba Bunge likubali kupitisha.
Waziri Mkuu alisema ni kweli kwamba kuna upungufu wa sukari nchini, ingawa pia upo udanganyifu kwa baadhi ya wafanyabiashara.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
Post A Comment: