Watanzania watakiwa kutumia miundombinu inayojengwa na serikali kikamilifu ili ilete manufaa kwa taifa zima
Makamu wa rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi, leo ametembelea
daraja la Mwalimu Nyerere, Kigamboni, ambapo amewataka watanzania kuwa
na imani na serikali yao kwenye miradi mbalimbali inayopangwa
kutekelezwa na wahakikishe miradi hiyo wanaitumia katika kuwanufaisha.
Balozi
Iddi amesema kuwa kuna miradi mingi ambayo serikali imepanga kutekeleza
ili kuhakikisha Tanzania bara na Tanzania visiwani zote kwa pamoja
zinakuwa na maendelo sawa na kupelekea Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
inakuwa nchi yenye uchumi wa kati.
Kwa upande wake meneja wa mradi wa ujenzi wa daraja la Nyerere
Eng.Karimu Mattaka amesema wamefunga mifumo maalum yakuchunguza shughuli
mbalimbali zitakazokuwa zinafanyika katika mradi huo ili kuhakikisha
wanaondoa masuala ya urasimu pindi mradi huo utakapoanza kukusanya
mapato.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
Post A Comment: