Beki wa kati kutoka nchini Ivory Coast na klabu ya Liverpool, Kolo
Toure ametishia kuondoka Anfield kama ataendelea kukalia benchi chini ya
utawala wa meneja Jurgen Klop.
Toure ambaye ni kaka wa kiungo wa klabu ya Man City Yaya Toure,
amesema ni vigumu kwake kuendelea kukaa kwenye klabu ya Liverpool ambayo
anashindwa kuitumikia kama ilivyokua matarajio yake.
Beki huyo ambaye aliwahi kuzitumikia klabu za Arsenal na Man City
ametishia kufanya hivyo huku mkataba wake ukitarajia kukamilika mwishoni
mwa msimu huu.
Hata hivyo meneja wa Liverpool, Jurgen Klopp ameonekana kuhitaji
kuendelea kuwa na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 35, japo amekua
hamtumii mara kwa mara katika mipango yake katika ligi pamoja na kwenye
michuano mingine.
“Ni jambo zuri kusikia hivyo kutoka kwa meneja mkubwa (kumbakisha Liverpool),
“Lakini kama nikipata nafasi kwenye kikosi, nitakuwa na furaha zaidi
lakini kama sitapata haitakuwa na jinsi,” Toure aliwambia BBC Sport.
Kolo Toure alijiunga na Liverpool mwaka 2013 akitokea Man City ambapo
alikabiliwa na wakati mgumu wa kupata nafasi ya kucheza mara kwa mara,
hali ambayo ilionyesha kumchosha na kulazimisha kuondoka klabuni hapo
mara tu, alipowasili meneja Manuel Pellegrini.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
Post A Comment: