ads

Kiungo mshambuliaji wa Azam FC Farid Malik amepelekwa klabu ya Deportivo Tenerife ya Ligi Daraja la Pili Hispania hapo jana tofauti na timu alizopangiwa hapo awali.


Wakala wa Farid, John Sorzano raia wa Venezuela aliyeishi sana nchini England amesema, ameamua mchezaji huyo aanzie timu ya Daraja la Kwanza Hispania ili kupata nafasi ya kucheza na kuinuka haraka, tofauti na mpango wa awali ambapo walitarajia angeznia timu mojawapo ya La Liga kati ya Las Palmas na Athletic ya Bilbao.

Farid atafanya majaribio hayo na kukaa huko kwa takribani wiki tatu na anatarajia kurejea nchini Mei 19 mwaka huu, ikiwa na maana kuwa atakosa mechi zote za Azam FC zilizobakia za msimu huu. 

Farid alikwenda Hispania Alhamisi akitoka kuichezea klabu yake, Azam FC katika mchezo wa marudiano hatua ya 16 Bora Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya wenyeji, Esperance walioshinda 3-0 mjini Tunis Jumanne.
DOWNLOAD APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD BONYEZA HAPA

ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: