Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto Bi Ummy
Mwalimu amewatoa wasiwasi wazee kuhusu changamoto mbalimbali
zinazowakabili ikiwemo upatikanaji wa huduma za afya .
Akizungumza na baraza la wazee wa Dar es salaam Bi. Mwalim amesema
serikali ya awamu ya tano imejipanga kikamilifu katika kutatua
changamoto mbalimbali zinazowakabili wazee ikiwemo kuanzisha mfuko wa
wazee ambao utawasaidia kupata mikopo ili kujikwamua kimaisha na pia
kutoa huduma za afya bure kwenye hospitali za serikali .
Bi Mwalim amesema wizara yake itapeleka sera ya sheria ya wazee
bungeni ili iweze kujadiliwa sera ambayo itasaidia sana kutatua
changamoto mbalimbali za zinazowakabili wazee.
Kwa upande wa wao baadhi ya wazee wametoa mapendekezo yao kwa waziri
ambapo wameombwa kuwepo na ushirikishwaji wa karibu wa wazee pamoja na
uwakilishi katika sekta mbalimbali .
Post A Comment: