ads

HATMA ya beki mahiri wa Simba, Abdi Banda inatarajiwa kujulikana leo baada ya uongozi kuipitia barua yake ya kujieleza.


Banda ameingia kwenye mgogoro na timu yake baada ya kumkatalia kocha Jackson Mayanja kufanya mazoezi mepesi ya kujiandaa kuingia uwanjani katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara dhidi ya Coastal Union Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.

Tukio hilo ndilo lililofanya uongozi wa Simba kumtaka aandike barua ya kujieleza kwa nini asichukuliwe hatua za kinidhamu.

Akizungumza jana, Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa klabu hiyo, Haji Manara alisema uongozi unatarajiwa kukutana leo kujadili barua yake na utaamua cha kufanya.

“Banda alitakiwa aandike barua na ameshaandika sasa kwa vile tulikuwa na mapumziko marefu ya sikukuu ya Pasaka nadhani kamati itakutana kesho (leo) na kisha itatoa uamuzi wa nini kitafanyika,” alisema.

Mayanja amemzuia Banda kufanya mazoezi na timu yake mpaka uongozi utakaamua juu ya suala lake.
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: