Mtangazaji wa Kipindi cha Wanawake Live,
Joyce Kiria ametoa kali ya mwaka kwa kueleza kuwa, akishibishwa vilivyo
na mume wake ‘chakula cha usiku’, haoni sababu ya kumsifia kupitia
mitandao.
Joyce ambaye amekuwa na kusumba na kumpa
sifa kemkemu mume wake kila atokapo kula ‘chakula’ hicho ameeleza kuwa,
haoni tatizo kufanya hivyo kwa kuwa kila mtu anajua ukiolewa lazima
upewe ‘chakula cha usiku’ na ushibe ndipo utaifurahia ndoa.
“Mi sioni ajabu jamani kwa sababu ni
vitu vya kawaida kabisa, nani asiyejua tumetoka kwa wazazi wetu kwa
ajili ya kufuata ‘chakula cha usiku?’ Kwa hiyo sioni hatari kwa kweli,
nitaendelea kumsifia mume wangu atakaponipa furaha, ” alisema Joyce.



Post A Comment: