ads
Belle 9 amedai kuwa kwenye muziki wake haamini kama collabo ni njia sahihi ya kumfikisha kimataifa zaidi.

Akizungumza na mtandao huu, Belle amesema wapo wasanii kadhaa walioweza kutoboa bila hata kufanya collabo na wasanii wa mataifa ya nje.
 
“Mimi nimefanya collabo na Joh Makini, I am proud kwa sababu ni msanii mkubwa ambaye anafanya vizuri ndani na nje. Joh is too expensive sio simple tu kufanya naye collabo,” amesema Belle.
 
“Kama unavyojua msanii mkali hawezi kurekodi na msanii mbovu, mimi naamini inawezekana. Mimi naamini collabo sio kitu kinawezeka kunifikisha International, sijui wasanii wenzangu wengine. 
 
"Kwa sababu mtu kama Gsan alishiriki mpaka cipher ya BET najua sio kawaida, sasa Gsan alifanya collabo na nani? Na ni washkaji ambao walikuwa level kubwa. 
 
"Mimi siamini collabo inaweza kunifikisha huko, yaani siamini katika collabo kwa sababu ningekuwa nimeshafanya na nimesharelease. 
 
"Lakini najua collabo ni maisha ya muziki ambayo inatokea ukafanya lakini mimi sijafikiria nijaribu kufanya ndio nifike huko,” aliongeza muimbaji huyo.
 
Belle anajiandaa kuachia video ya wimbo wake ‘Shauri Zao’ iliyoongozwa na Hanscana.
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: