ads
Staa wa filamu bongo ,Halima Yahya Amedai kutoshwa na mwanaume aliyemuachanisha na mumewe ambaye alikuwa ni bosi wake katika kampuni moja iliyopo kinondoni jijini dar es salaam


chanzo cha kuaminika kilichoomba hifadhi ya jina lake kinadai kuwa , baada ya davina kuzinguana na mumewe kisa huyo bosi (hifadhi jina lake kwa sasa) alifunguliwa ofisi maeneo ya kinondoni jijini dar kisha maisha yakaendelea.


“Si unakumbuka kuna yule mwanaume ambaye ndiye alimzuzua Davina hadi akaachana na mumewe? Basi baada ya pale Davina alifungiliwa ofisi yeye na Mike (Sangu) iliyokuwa inajihusisha na mambo ya TV ya mtandaoni, mambo yakawa bambam, akasahau hata machungu ya ndoa yake kuvunjika.

“Lakini sasa hivi mambo yameharibika, yule kibosile katibuana na Davina, kaamua kuchukua kila kitu katika ofisi ile na kuiacha tupu.

Mike ambaye ndiye aliyemshawishi Davina waanzishe hiyo ofisi sasa hivi yuko zake mkoani anampigia debe mgombea wake,” kilidai chanzo hicho na kuongeza:

“Sasa hivi Davina anahaha, anajuta kuachana na mumewe.”

Davina alipovutiwa waya na kuulizwa juu ya madai ya kutoswa na mwanaume aliyevunja ndoa yake alisema amechoshwa na maneno ya watu kwani hajawahi kuwa na uhusiano na bosi wake huyo.

“Mh! Watu wananitungia habari jamani mimi sipendi kwa sababu hawajui tu wanavyoniharibia, sijawahi kuwa na uhusiano na bosi wangu, kuhusu kazi mbona bado naendelea na hivi ninavyokwambia naelekea hapo kazini,” alisema Davina.

Akizungumzia ishu hiyo, Mike Sangu aliyekuwa akifanya kazi ofisi moja na Davina alisema: “Hayo mambo ya Davina kuwa na uhusiano na mkurugenzi wetu siyajui, ninachojua kwa sasa tumesimama kidogo kwa sababu tunafanya usaili wa watu ili tufungue televisheni kwa ujumla kwani mwanzo ilikuwa TV Online na hata huyo Davina tumemuambia alete CV,” alisema Mike.

ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: