ads
Biashara ya ngono imezidi kushamiri wakati huu vikao vya kumchagua mgombea uraisi kupitia chama cha mapinduzi (CCM)


Uchunguzi uliofanywa  katika baadhi ya kumbi kama  Club Maisha, Club Laazizi na Matei Lounge, Chako ni Chako, umebaini kuwapo idadi kubwa ya kina dada wakiwa wamevaa nusu uchi.

Katika maeneo ya katikati ya mji wa Dodoma zilikuwapo hekaheka za wasichana wanaojiuza ambao walionekana wakitafuta wateja bila ya wasiwasi wowote na wengine walisikika wakisema  wako kibiashara na siyo kuuza sura.

Eneo maarufu la Chako ni Chako kuanzia jioni mpaka usiku kucha  akina dada hao wamekuwa wakijazana hadi kwenye taa za kuongozea magari huku wakitafuta wateja wenye magari.

Baadhi yao ambao hawakutaka kutaja majina yao halisi mmoja wao alisema,‘’Kaka sema una shilingi ngapi habari ya majina unataka kutupeleka wapi…?

‘’……wewe unaona shimo limetema hapa kila nikigeuka mwanaume na wanatoa ‘mpunga’ nadhani huyu rais ajaye atakuwa na neema.’’

Dada mwingine ambaye aliyekuwa   Dodoma Carnival karibu na Kituo Kikuu cha Mabasi, alisema ametoka Arusha akiwa na marafiki zake kwa lengo la kuwafuata wateja wa msimu walioko Dodoma.

Alisema hadi sasa ana   siku tatu akiwa  Dodoma na tayari amekusanya zaidi ya Sh 700,000 huku akiwatumia madalali  ambao huwaunganisha kwa wateja
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: