ads

WAJUMBE watano wa kamati ya utendaji ya Simba, watalazimika kukaa kando kupisha mabadiliko yatakayofanyika baada ya klabu hiyo kuingia katika mfumo wa hisa.


Kaimu Rais wa Simba, Dokta Salim Abdallah alisema, baada ya kamati ya zabuni kumtangaza mshindi wa mchakato wa uwekezaji wa klabu hiyo, wajumbe watano wa kamati ya utendaji watapunguzwa ili kubakia na saba ambao wataingia kwenye bodi itakayoundwa.

"Baada ya kamati ya zabuni kumtangaza mshindi, kamati ya utendaji itaanza kazi mara moja kutangaza wajumbe saba ambao wataungana na wajumbe saba upande wa mwekezaji, kuunda bodi ya kusimamia klabu yetu," alisema Abdallah.

"Wajumbe wa kamati ya utendaji wapo 12 ambao hawawezi kuingia wote kwenye bodi hivyo baadhi yetu hawatopata nafasi ya kuingia."
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: