
Subscribe ndio neno gumu zaidi kwa wabongo kuliko kutafuna jiwe kama ilivyo kwa Waingereza kutamka Mwanjelwa..husema Monjela
Pamoja na vionjo hivyo..kwenye Simba Day ya mwaka huu ntakuja na style tofauti ya kutambulisha wachezaji...njoo ushuhudie mwenyew..usingoje kuhadithiwa ni Jtano hii pale dimba la Taifa... #SimbaDay #KibingwaZaidi π΅πͺπ΅πͺ
Serikali yatoa tamko kuadimika mafuta ya kula nchini
Waziri Kigwangalla atetea ununuzi wa ndege
Zitto Kabwe amshauri Job Ndugai
Bunge lataka tende zifutwe kodi mfungo wa Ramadhani
Mo Dewji afunguka jinsi anavyopiga pesa kupitia kilimo
SERIKALI imetahadharisha kuwa mvua kubwa zinazotarajiwa kunyesha katika maeneo mbalimbali nchini kuanzia mwezi ujao.
Pia imesema mvua kubwa zilizotabiriwa na Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA) kwa msimu huu wa mvua za vuli unaoanzia Oktoba hadi Desemba, zimesababisha mafuriko, vifo, magonjwa ya mlipuko, uharibifu wa mazao, mazingira na miundombinu.
Aidha, serikali imetahadharisha kuwa madhara hayo yanaweza kuongezeka endapo hatua stahiki hazitachukuliwa kwa kuzingatia ushauri wa kitaalamu.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia Watu Wenye Ulemavu, Stella Ikupa, alitoa tahadhari hiyo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye Ukumbi wa Idara ya Habari na Elimu ya Bunge mjini hapa.
Alisema tayari athari zimejitokeza katika maeneo yanayopata mvua hizo ya Ukanda wa Ziwa Victoria, Nyanda za Juu Kaskazini Mashariki, Pwani ya Kaskazini na maeneo ya kaskazini mwa mkoa wa Kigoma.
Alizitaka kamati za maafa kuanzia ngazi ya kijiji na mitaa hadi kitaifa, kuchukua hatua za kuzuia, kupunguza madhara na kujiandaa kukabiliana na maafa endapo yatatokea tena.
Ikupa alisema kuwa kwa mujibu wa sheria, maafa hushughulikiwa kuanzia ngazi ya chini, mtu binafsi akiwa ndiyo ngazi ya kwanza akifuatwa na kaya, kijiji na kuendelea, hivyo kila ngazi ihakikishe inajiandaa vya kutosha kutekeleza wajibu wake.
"Serikali inatoa pole kwa wananchi walioathirika na mvua hizo," Ikupa alisema, "tunaendelea kutoa tahadhari kwa umma na kuzielekeza taasisi mbalimbali kuchukua hatua stahiki kwa lengo la kupunguza madhara yoyote yanayoweza kujitokeza na kujiandaa kukabili na kurudisha hali bora zaidi ya ile ya awali."
Alizipongeza halmashauri zote kwa hatua ambazo zimezichukua hasa kwa maeneo ambayo mvua hizo zilisababisha maafa.
Kwa upande mwingine, Naibu Waziri huyo aliwataka wananchi kutupa fursa chanya ya mvua hizo kwa shughuli za maendeleo ya kilimo, kuandaa mabwawa, malambo, kuvuna maji na kupanda mazao yanayohitaji maji mengi kama vile mpunga, uzalishaki samaki na kuandaa malisho.
Post A Comment: