KLABU za Gor Mahia inayoshiriki Ligi Kuu ya Kenya na St. George ya Ethiopia, zinatajwa kumwania mshambuliaji wa kimataifa wa Simba kutoka Burundi, Laudit Mavugo, imeelezwa.


Hata hivyo, Akizungumza na gazeti la Nipashe jana, Kaimu Rais wa Simba, Salim Abdallah "Try Again" amesema kuwa hakuna mchezaji hata mmoja atakayeachwa na hiyo inatokana na ripoti ya kiufundi waliyokabidhiwa na Kocha Mkuu, Joseph Omog.

Salim alisema jana kuwa chini ya uongozi wake, hakutakuwa na kiongozi atakayesajili mchezaji au atakayependekeza nyota kuachwa, kwa sababu jukumu hilo liko chini ya Omog na wasaidizi wake tu.

"Kila kitu kinaendeshwa kwa kufuata kanuni na taratibu, Simba ni taasisi na ni kubwa kuliko mchezaji au kiongozi, ni lazima hilo liheshimiwe," alisema kiongozi huyo ambaye anakaimu nafasi iliyoachwa na Evans Aveva, anatuhumiwa kutumia vibaya fedha za klabu.

Taarifa zilizopatikana jijini zinasema kuwa kuna mazungumzo yasiyo rasmi yanaendelea na lengo la kufanya hivyo ni kutaka kushawishi mshambuliaji huyo aachwe kwa ajili ya kukwepa kulipa ada ya uhamisho kwa sababu mshambuliaji huyo bado ana mkataba na Simba.

"Mimi najua St. George ndiyo wanamtaka, na hawakuanza sasa, ila wanaonyesha wanataka kumsajili kupitia mlango wa nyuma, na hili haliwezekani," alisema kiongozi mmoja wa Simba.
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: