ads

PAMOJA na wakati mgumu wanaopitia kwa sasa kutokana na kuwa na wachezaji waandamizi ambao ni majeruhi, Yanga bado imetamba kutetea ubingwa wao msimu huu.


Msimu huu Yanga inayodhaminiwa na kampuni ya Sportpesa imekosa huduma ya nyota wake, Amisi Tambwe ambaye hajacheza mchezo wowote wa ligi kuu msimu huu na Donald Ngoma aliyecheza michezo ya mwanzoni, wote hao ni majeruhi.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Kocha msaidizi wa timu hiyo, Shadrack Nsajigwa, alisema kuwa pamoja na changamoto hiyo, bado wanauwezo na watapambana kuhakikisha wanatetea ubingwa wao.

“Kinachotia moyo, pamoja na kuwa na majeruhi na changamoto nyingine, bado tumeweza kupambana na kutopoteza mchezo,” alisema Nsajigwa.

Alisema kuwa hiyo inawapa moyo kutokana na wachezaji wao kupambana na muda si mrefu mabingwa hao watetezi watarudi kwenye kiwango chao.

“Bado kuna michezo mingi mbele yetu, ukiangalia timu inazidi kuimarika na wachezaji wetu majeruhi wakipona kabisa nguvu itaongezeka zaidi,” alisema Nsajigwa.

Yanga wanaendelea na mazoezi kujiandaa na mchezo wao ujao dhidi ya Mbeya City utakaochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru Novemba 19.

Kikosi hicho cha Kocha George Lwandamina, kipo nafasi ya tatu nyuma ya Simba na Azam ikiwa na pointi 17 sawa na Mtibwa Sugar inayoshika nafasi ya nne.

Simba inaongoza ligi ikiwa na pointi 19 sawa na Azam lakini yenyewe ikiwa na uwiano mzuri wa mabao ya kufunga na kufungwa.
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: