ads

Dk Louis Shika aliyetangazwa kununua nyumba za Mfanyabiashara mkubwa Lugumi zilizopo Mbweni jijini Dar es Salaam kwenye mnada uliyofanyika leo Novemba 9,2017 amekamatwa na polisi kwa kile ninachoelezwa kuharibu mnada huo kwa kushindwa kutoa asilimia 25 ya gharama za nyumba hizo.


Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya udalali ya Yono ambayo ndio iliyoendesha mnada huo, Scolastica Kevela amethibitisha tukio hilo na kueleza kuwa mnunuzi huyo alipotakiwa kutoa kiasi cha fedha 'kitanguliza malipo' hakuwa na fedha hizo huku akidai zinatoka Kenya.

"Ni kweli tumempeleka polisi, tulimwambia atoe asilimia 25 ya mwanzo kama ambavyo sheria inataka akawa hana.. na kudai hela hiyo inatoka Kenya tusubiri leo au kesho, wakati masharti hayasemi hivyo na tulimtangazia kabla ya mnada, inaonekana hakujiandaa tukaamua tumpeleke polisi kwa kuaribu mnada", amesema Kevela

Mnada wa nyumba hizo umelazimika kurudiwa upya ili kuweza kupata mnunuzi halali wa mali za Lugumi.
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: