ads

MSIMU uliopita katika mzunguko wa kwanza, Shiza Kichuya aliifungia Simba, mabao tisa (mechi 15), rekodi inayokaribia kuvunjwa na Emmanuel Okwi aliyefunga mabao nane kwa mechi tisa, akiwa amebakiza mechi sita ili zifike 15.


Kwa rekodi hiyo, Okwi yupo nyuma bao moja dhidi ya Kichuya aliyefunga mabao matano kwa msimu huu,kabla ya kupisha usajili wa dirisha dogo kama ilivyokuwa mwakajana.

Okwi alijiunga na Simba msimu huu, ujio wake ulizua mjadala mkubwa,huku baadhi wakiamini  jezi namba 25, anayoitumia Kichuya angepewa mkongwe huyo ambaye kwa sasa anatumia jezi namba saba.

Hata hivyo Kichuya alionekana kujiandaa kisaikolojia kuhusiana na jezi namba 25 aliyokuwa anatumia Okwi zamani, pamoja na kujipanga kiuwezo ili asikae benchi kama ilivyokuwa matarajio ya wengi.

Kichuya amewahi kukaririwa akisema "Naheshimu uwezo wa Okwi, kwani nimemuona akicheza na nimezikuta rekodi zake Simba, hilo siyo sababu ya mimi kukaa benchi, bali atageuka somo kujua amefikaje kwenye mafanikio hayo, ili na mimi nifuate nyayo zake,"alisema.

Simba ndiyo ilikuwa inaongoza kwa pointi dhidi ya Yanga, kabla ya kupisha usajili wa dirisha dogo kama ilivyo kwa sasa ambapo wanaongoza kwa pointi 19 sawa na Azam, isipokuwa kwa uwiano wa mabao.

Yanga ni Donald Ngoma ndiye alikuwa anaongoza kwa mabao sita kwa mechi 15, alizokuwa amecheza mzunguko wa kwanza, msimu uliopita, rekodi inayokaribia kuvunjwa na Ibrahim Ajib aliye na mabao matano katika mechi tisa.
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: