Waziri wa Maliasili na Utalii, Hamisi Kigwangalla amefuta vibali vyote vya uwindaji kwa kampuni kuanzia jana Oktoba 22,2017 na kutoa siku 60 kwa watendaji ili waratibu mchakato upya utakaowezesha vitalu kugawiwa kwa mnada.


Dk Kigwangalla pia amemwagiza katibu mkuu wa wizara hiyo, ndani ya muda mfupi kuwaandikia Hazina ili kuzichukua hoteli 10 kati ya 17 zilizobinafsishwa ambazo zimeshindwa kutimiza masharti.

Ametoa maagizo hayo  alipohitimisha mazungumzo na wadau wa sekta ya utalii na maliasili aliokutana nao mjini  Dodoma.

β€œKwa mamlaka niliyonayo katika sheria, natamka kwamba, nafuta rasmi vibali vyote vya uwindaji kwa kampuni vilivyotolewa na wizara yangu kwa mwaka huu. Pia, naagiza watendaji wote wanaosimamia hili wahakikishe wanaandaa mchakato ndani ya siku 60 ili mnada ufanyike na uwe wa uwazi,” ameagiza Dk Kigwangalla.

Kuhusu vitalu vyenye migogoro vikiwemo vya Loliondo na Natroni, ameagiza visigawiwe hadi migogoro itakapokwisha.

"Kwenye hili la hoteli, nataka katibu uwasiliane na mamlaka husika, ikiwemo Msajili wa Hazina ili ndani ya siku 60 uje na majibu tutangaze kwa wawekezaji watakaokwenda na masharti," amesema.
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: