
Subscribe ndio neno gumu zaidi kwa wabongo kuliko kutafuna jiwe kama ilivyo kwa Waingereza kutamka Mwanjelwa..husema Monjela
Pamoja na vionjo hivyo..kwenye Simba Day ya mwaka huu ntakuja na style tofauti ya kutambulisha wachezaji...njoo ushuhudie mwenyew..usingoje kuhadithiwa ni Jtano hii pale dimba la Taifa... #SimbaDay #KibingwaZaidi 🇵🇪🇵🇪
Serikali yatoa tamko kuadimika mafuta ya kula nchini
Waziri Kigwangalla atetea ununuzi wa ndege
Zitto Kabwe amshauri Job Ndugai
Bunge lataka tende zifutwe kodi mfungo wa Ramadhani
Mo Dewji afunguka jinsi anavyopiga pesa kupitia kilimo
KOCHA wa Arsenal, Arsene Wenger, ameelezea umuhimu wa mchezaji wake, Alexis Sanchez, kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Chile, kwamba ni kama ilivyokuwa kwa Lionel Messi, Zinedine Zidane na David Beckham, kwa timu zao.
Wenger alitoa kauli hiyo muda mfupi baada ya Chile kushindwa kufuzu michuano ya Kombe la Dunia, inayotarajiwa kufanyika mwakani nchini Urusi.
Chile ya Sanchez imeshindwa kufuzu michuano hiyo, baada ya kupokea kipigo cha 3-0 dhidi ya Brazil katika mechi ya mwisho iliyochezwa Jumanne iliyopita.
Wenger, ambaye timu yake itarejea Ligi Kuu kwa safari ya kwenda Watford leo, alisema Sanchez ni miongoni mwa kundi la wachezaji ambao timu zao za taifa zimekuwa zikiwategemea, sawa na Zidane ilivyokuwa kwa Ufaransa, Beckham kwa Uingereza na Messi kwa Argentina.
“Naweza kusema katika kila kizazi kuna mchezaji anayebeba presha ya matarajio ya taifa lake,” Mfaransa huyo alisema.
“Kwa Ufaransa alikuwa Zidane. Uingereza alikuwa Beckham. Tulikuwa na wachezaji wengine kwenye timu, lakini alikuwa Beckham. Kwa nini siyo Steven Gerrard? Sijui. Lakini alikuwa Beckham.
“Kwa Chile ni Sanchez. Kwa Argentina ni Messi. Inaonekana katika kila timu ya taifa yupo mmoja anayebeba presha na kulinda timu yote kwa ujumla.
“Ni mtu anayependa majukumu. Wanapenda kuwa mstari wa mbele. Lakini kwa ujumla hili lina maana gani? Inamaanisha ni lazima wakubaliane na kushindwa pia.”
Sanchez (28), anahusishwa na tetesi za kuondoka Arsenal kwa muda mrefu, wakati nyota huyo akiwa kwenye mwaka wa mwisho kwenye mkataba wake na klabu hiyo.
“Yuko sawa katika kipindi kigumu. Chile wameshinda Copa America mara mbili na sasa wameshindwa kwenda Kombe la Dunia,” alisema Wenger.
“Sanchez atakuwa na umri wa miaka 29 mwisho wa mwaka huu, kwa hiyo Kombe lingine la Dunia atakuwa na miaka 33. Anatarajia kwenda. Kwa yakini ni jambo ambalo limemuumiza.
“Lakini naamini kucheza katika kiwango chake cha juu ni sehemu pia ya kukubali changamoto.”
Post A Comment: