Subscribe ndio neno gumu zaidi kwa wabongo kuliko kutafuna jiwe kama ilivyo kwa Waingereza kutamka Mwanjelwa..husema Monjela
Pamoja na vionjo hivyo..kwenye Simba Day ya mwaka huu ntakuja na style tofauti ya kutambulisha wachezaji...njoo ushuhudie mwenyew..usingoje kuhadithiwa ni Jtano hii pale dimba la Taifa... #SimbaDay #KibingwaZaidi 🇵🇪🇵🇪
Serikali yatoa tamko kuadimika mafuta ya kula nchini
Waziri Kigwangalla atetea ununuzi wa ndege
Zitto Kabwe amshauri Job Ndugai
Bunge lataka tende zifutwe kodi mfungo wa Ramadhani
Mo Dewji afunguka jinsi anavyopiga pesa kupitia kilimo
WAKATI amri za Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema, na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa, kuhusiana na kusakwa, kukamatwa na kuchukuliwa hatua kwa polisi walioingia mitaani kupiga raia kwa siku tatu mfululizo-
Eneo la Ukonga jijini Dar es Salaam zikiendelea kusubiria utekelezaji wake, wahusika wamezidi kuwekwa kikaangoni baada ya kuibuka maswali takribani 10 kuhusiana na tukio hilo.
Baadhi ya maswali kuhusiana na tukio hilo ni pamoja na kujua askari hao walipata wapi kibali cha kwenda mitaani kufanya operesheni ya kupiga watu na sababu za kutopatikana kwao kirahisi ilhali baadhi yao wakidaiwa kufika na magari ya jeshi hilo, hivyo madereva wao kuwa na nafasi ya kuwabaini wahusika.
Akizungumza na gazeti la Nipashe jana, Kamanda Mambosasa alitolea ufafanuzi baadhi ya maswali hayo, ikiwamo kueleza kuwa askari waliofanya fujo na kuwajeruhi wananchi hawakutumwa na jeshi hilo bali walijipeleka baada ya kumalizika kwa kazi ya kundi la askari wa awali waliokuwa wametumwa rasmi.
"Wapo askari ambao tunawatambua, tuliwatuma kwenda kuwasaka wahalifu wa tukio hili la kuuawa kwa askari wetu wa FFU ambao walimaliza kazi yao majira ya saa 5:00 usiku," alisema Mambosasa.
Juzi, Mjema alitembelea eneo la Ukonga Mombasa na kuwapa pole wananchi waliokumbana na vipigo kutoka kwa askari wasiofahamika wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), ambao wanadaiwa kutembeza vipigo kwenye mitaa ya eneo hilo kwa siku tatu mfululizo kwa kile kilichoelezwa kuwa ni msako dhidi ya wauaji wa askari mwenzao, Charles Yanga.
Kwa mujibu wa polisi, askari huyo alikutwa amekufa huku mwili wake ukiwa na majeraha yaliyoonyesha alipigwa na kitu chenye ncha kali.
Akizungumza na wananchi waliokuwa wakiandamana kulaani vipigo dhidi yao, Mjema ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama katika wilaya yake, alitoa pole kwa waathirika na kumtaka Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi wa Ilala kuhakikisha askari wote waliohusika kuwatembezea vipigo wananchi wasio na hatia wanachukuliwa hatua.
Mjema aliagiza pia wote walioumia waorodheshwe majina ili wakapate matibabu wakati hatua zingine zikiendelea kuchukuliwa; uamuzi ambao uliibua shangwe kubwa kutoka kwa wananchi waliokuwa wakimsikiliza.
“Jambo ambalo limefanyika kwa siku tatu halikubaliki. Kama kulikuwa kuna matatizo, kati ya askari na raia, kulikuwa kuna eneo la kupeleka matatizo hayo,” alisema na kuongeza:
“Kama kuna askari aliyekuwa amepatikana ameshafariki dunia, utararibu ulikuwa uchunguzi ufanyike ili kujiridhisha. Baada ya hapo, wale ambao wangetambulika ndio wangechukuliwa… lakini kwa hili, halikubaliki. Kwa maana hiyo, nasema hivi, askari wote walioshughulika kufanya jambo hili, RPC upo, wachukuliwe hatua za kinidhamu, na huku barabarani sitaki kuona FFU yeyote anasumbua wananchi.”
Kwa mujibu wa baadhi ya wananchi katika maeneo ya Ukonga, ikiwamo Mombasa, Banana na barabara kuelekea Kwa Mkolemba, Moshi Bar na Kwa Diwani, askari walikuwa wakiwapiga watu ovyo, hasa nyakati za usiku na kuwaumiza baadhi yao, huku pia biashara katika maeneo hayo zikifungwa.
Mbali na kitendo hicho kumkera Mjema, pia Kamanda Mambosasa alitoa taarifa juzi ulioonyesha kuwa jeshi hilo haliungi mkono askari waliofanya vitendo hivyo baada ya kuwataka wananchi wajitokeze kuwabaini askari waliopiga watu na mwishowe hatua zichukuliwe dhidi ya wahusika.
MASWALI 10 PASUA KICHWA

Wakizungumza na Nipashe kwa nyakati tofauti, baadhi ya wananchi walihoji maswali kadhaa yakiwamo takribani 10 kuhusiana na tukio hilo, baadhi yake ikiwa ni uhalali wa askari ambao ni walinzi wa raia na mali zao kutenda tukio hilo.
Miongoni mwa maswali hayo ni mosi; nani aliwapa kibali wahusika kufanya operesheni ya kupiga watu ovyo mitaani; pili ni hoja kuwa kama hawakutumwa, je, wahusika walitoa wapi ujasiri wa kufanya yale yanayofanana na vikundi vya kibabe kama ‘panya road’ ambavyo ndivyo hufahamika kuwa huwashambulia raia wasio na hatia kwa nia ya kuwapora?
Swali la tatu ni je, kwa nini askari hao hawakutoa nafasi kwa wapelelezi wenye ujuzi ndani ya jeshi hilo kufanya kazi yao ili kuwabaini watuhumiwa sahihi wa mauaji ya askari mwenzao? Nne, ni je, askari walioshiriki kutembeza vipigo mitaani walitumia magari gani? Swali la tano, mafuta na vitendea kazi vingine kwa ajili ya kufanyia operesheni hiyo walipata wapi? Swali la sita ni je, kama ‘difenda’ za polisi zilihusika katika kufanikisha operesheni ya kuwapiga wananchi wasio na hatia, je, ziliendeshwa na kina nani?
Saba ni je, kwa nini madereva wa ‘difenda’ zilizokuwa zikiwabeba askari hao wasibanwe kuwataja wenzao? Kama hiyo haitoshi, swali la tisa ni ukweli kuwa sifa kuu ya askari ni kuwa na nidhamu, hivyo kwanini wahusika hawamtii DC Mjema na Kamanda Mambosasa kwa kujitokeza na kueleza kile kilichotokea bila shuruti? Kumi ni je, iweje polisi ishindwe kuwajua askari hao waliopiga raia mitaani kwa siku tatu mfululizo? Swali la 11 ni je, askari waliofanya vitendo hivyo hawakujua kuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Simon Sirro, aliahidi kuwa kipaumbele chake kikubwa ni nidhamu chini ya uongozi wake?
“Swali lingine la kujiuliza ni je, askari waliowashambulia raia wasio na hatia hawakujua kuwa IGP Sirro husisitiza kuwa ni marufuku kwa askari kuonea raia wasio na hatia?” alihoji mmoja wa wananchi waliozungumza na Nipashe kwa sharti la kutoandikwa majina yao.
UFAFANUZI WA MAMBOSASA
Alipotafutwa na Nipashe jana jioni kuzungumzia sakata hilo, Kamanda Mambosasa alisema bado hawajawapata askari wanaodaiwa kuwajeruhi wananchi eneo la Ukonga jijini kutokana na kile alichosema kuwa ni wananchi kuogopa kutoa ushirikiano kwao.
Kamanda Mambosasa alisema Jeshi la Polisi linaendelea kuwatafuta askari hao na kusisitiza rai ya kuwataka wananchi watoe ushirikiano kwao.
Aidha, alisema askari waliofanya fujo na kuwajeruhi wananchi hawakutumwa na jeshi hilo bali walijipeleka wenyewe baada ya wale wa awali waliotumwa kukamilisha kazi yao.
"Wapo askari ambao tunawatambua, tuliwatuma kwenda kuwasaka wahalifu wa tukio hili la kuuawa kwa askari wetu wa FFU ambao walimaliza kazi yao majira ya saa 5:00 usiku," Kamanda Mambosasa alisema na kufafanua zaidi:
"Baada ya kurudi, wapo waliokwenda tena kwa wananchi wakiwa wamejipangia kazi wenyewe… ambao waliingia mtaani kufanya fujo kwa wananchi. Jeshi halikuwatuma."
Kamanda Mambosasa aliwataka wananchi wajitokeze kuwasaidia katika utambuzi wa askari waliofanya vitendo hivyo.
"Tunawaomba wananchi watupe ushirikiano ili tuweze kuwatambua kwa sababu baada ya tukio la kuumizwa wananchi, yupo askari alikamatwa lakini wananchi waliojeruhiwa walimtetea kuwa siye aliyefanya fujo siku hiyo bali aliwatetea wakati wanapigwa,” alisema Kamanda Mambosasa.
Post A Comment: