Kiongozi wa Muungano wa Upinzani, Nasa, nchini Kenya, Raila Odinga, amepuuzia uchaguzi wa marudio wa Urais uliofanyika jana nchini humo na kudai kwamba haukuwa wa halali, hivyo anajiandaa kwa uchaguzi mwingine.


Odinga amesema, uchaguzi huo haukuwakilisha Wakenya walio wengi hivyo yeye anajiandaa kwa uchaguzi mwingine utakaofanyika baada ya siku 90.

Akizungumza kwa mara ya kwanza tangu kufanyika kwa uchaguzi huo wa marudio, Odinga amesema kwamba uchaguzi huo mwingine utafanyika hata kama malalamiko yao hayatashughulikiwa na Tume ya Uchaguzi IEBC.

Odinga amesisitiza kwamba, muungano wa upinzani, hauutambui uchaguzi huo wa marudio kufuatia kuvurugika katika baadhi ya maeneo nchini humo.

Odinga aliamua kujitoa kwenye kinyang'anyiro cha uchaguzi siku chache kabla ya kufanyika kwa uchaguzi huo wa marudio uliofanyika hana Oktoba 26 baada ya ule wa Agosti 08 kutenguliwa na mahakama kwa madai kwamba ulikuwa na dosari nyingi.
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: