England.Kocha Manchester United, Jose Mourinho ni mwenye furaha baada ya taarifa kuweka wazi kiungo wake Paul Pogba atakuwa fiti kuzivaa Arsenal na Manchester City.


Pogba yupo nje ya uwanja kwa zaidi ya mwezi sasa huku akitarajiwa kuwa fiti kuanza kucheza mechi itakapofika Desemba.

Habari njema kwa kocha Mourinho ni kwamba Pogba atarudi katika mwezi ambao kawaida umekuwa na mechi nyingi sana zinazotoa mwanga wa kutambua mbio za kuwania ubingwa zilivyo.

Man United itakipiga na Arsenal, Desemba 2 huko uwanjani Emirates na siku nane baadaye, yani Desemba 10 watakuwa Old Trafford kuwakaribisha mahasimu wao wakuu, Man City.

Man United juzi Jumamosi ilikubali kipigo cha kwanza kwenye Ligi Kuu England ilipochapwa na Huddersfield na kichapo hicho kinawafanya waachwe kwa pointi tano na wapinzani wao katika mbio za michuano hiyo, Man City.
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: